MAMBO MATATU MUHIMU KANISANI.

ZAIDI HAPA

Friday, January 12, 2024

MAMBO MATATU MUHIMU KANISANI.

 


MAMBO MATATU MUHIMU KANISANI.

 Paulo mtume anasema hakuna awezaye kuweka msingi mwingine isipokuwa sote tunajenga katika msingi huu. Lakini kila ajengaye ni lazima awe makini na kazi yake. Msingi ukiwa ni Kristo,basi ni dhahiri Kristo atakuwa ni kiini cha injili na mafundisho yote ya kanisani pamoja na uimbaji wake . ( 1 Wakorintho 3:11)

 Hivyo kanisa ambalo halimhubiri Kristo ipasavyo lipo nje ya msingi wa kweli. Wakati kanisa likiwa na msingi Kristo,basi kanisa la Kristo linapaswa kuweka mkazo katika mambo muhimu yafuatayo;

 1. Roho mtakatifu na karama zake 

 Kwa kuwa Roho mtakatifu ndiye mtendaji mkuu wa Neno. Anapaswa apewe nafasi ya kutosha katika kila ibada inayofanyika,ili awasaidie waabuduo wakaabudu katika Roho na kweli.

 Lakini Roho mtakatifu afundishwe mara kwa mara, pamoja na karama zake. Kanisa la Kristo ni lazima liwe na ibada za ujazo katika Roho mtakatifu mara kwa mara kwa maana Roho akifurika,anaimarisha huduma. Kama alivyoimarisha huduma za mitume wakati wa kanisa la kwanza pale walipobatizwa katika Roho ndipo walipoweza kutoka na kuhubiri kote kote.

 2. Fundisho la imani (Yoh.8:31-32)

 Msingi wa fundisho la imani ni kufundisha kweli ya wokovu. Hapo ndipo kufanyika “ waberoya ” ( Matendo 17:11). Ni vyema katika kila fundisho kukawa na application ya kile kilichofundishwa . Neno “ application ” ni namna gani neno hilo lililofundishwa linaweza kuwekwa kwenye maisha. Mfano chukulia kwamba mhubiri amefundisha kuhusu kuinuliwa kiuchumi,Sasa application ni pale atakapoeleza ni namna gani mtu anatakiwa afanye ili ainuliwe kiuchumi.

 3. Maombi, maombezi, kufunguliwa na ushauri wa kibiblia kila ibada

 Kanisa la Kristo limejengwa katika msingi wa maombi kila siku pamoja na  maombezi. Tukisema “maombi” tuna maana waamini lazima wawe waombaji na  lazima waombewe. Tunamshinda shetani na nguvu zake kwa njia ya maombi na maombezi, tena kupitia maombi kanisa linapata nguvu ya kiroho ya kusonga mbele ipasavyo.

 KUMBUKA:

 ibada za maombi ya kufunga zinatakiwa kupewa kipaumbele cha kwanza kwa maana hapo ndipo Roho mtakatifu mara nyingi husema na watu wake ( Matendo 13:2). Kanisa likipoa katika maombi litachezewa na nguvu za giza sana.

 Kwa maombi , maombezi na ushauri  +255 714890889

Whats app  namba +255 762756542

 

 

Tuandikie 'Maoni Yako' Hapa
Share :
Facebook Twitter

 

ads

Back To Top