TOBA NA MSAMAHA WA DHAMBI

ZAIDI HAPA

Friday, January 12, 2024

TOBA NA MSAMAHA WA DHAMBI

 


TOBA NA MSAMAHA WA DHAMBI

3.1. MAANA YA TOBA

Andiko letu la msingi ni; Mithali 28:13; *"Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema."*

Tunaona katika maandiko habari za kupata rehema. Rehema ni nini?

Rehema ni msamaha ambao mtu hastahili kuupata yaani akiangalia maisha yake anaona kabisa anastahili hukumu. Nimeanza na kuzungumzia rehema sababu hatuwezi kuongelea toba kama hatutagusa rehema na msamaha.

Neno linasema afichae dhambi zake hatafanikiwa. Ukificha dhambi zako kwanza unajidanganya mwenyewe, sababu Mungu hafichwi na kitu chochote. Lakin badae akaendelea kusema bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema..

Kuna maneno haya...

Kuungama na

Kuacha na

Rehema.

Kuungama maana yake ni kukiri na kukubali makosa yako. Tunajua kwamba ukikiri makosa yako haina maana umeacha, sababu unaweza ukakiri leo, kesho ukarudia. Unaweza ukaungama leo kesho ukarudia tena. Kwahiyo kukiri ni mojawapo ya hatua ya kuelekea kwenye toba ya kweli.

Lakini tunaona mwandishi anasema ukiziungama na kuacha; ...maana yake usiishie kwenye kuungama tuu usiishie kwenye kukubali tu bali baada ya kukiri unatakiwa kuacha sasa na usifikirie kurudia wala usirudie.

Halafu mwishoni akamalizia kwa kusema atapata rehema. Unaweza kujiuliza sasa toba ndo iko wapi hapo??

Ukishakubali makosa yako unatakiwa kuacha, na kuacha ni kuamua na ukiamua kuacha then utapata msamaha yaani ondoleo la dhambi. Msamaha ni ondoleo la dhambi na makosa.

Toba ni nini?

Toba ni kugeuka kwa lugha nyingine ni kuacha; yaani, kama ulikuwa unaelekea kaskazini then unaamua kugeuka na kuelekea kusini, hyo ndo toba. Toba sio maneno matupu kama kuungama toba ni vitendo. Unapotubu unahamishwa kutoka kwenye ufalme wa giza kupelekwa kwenye ufalme wa nuru.

Matendo ya Mitume 11:18; *"Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima."*

Unaona hapo, nagundua kitu! ...kumbe toba inaleta uzima. Hebu tuangalie maandiko matakatifu tena yanaseaje!

Warumi 10:9-10; *"Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu."*

Mstari wa 10 unasema …kwa moyo, mtu huamini hata kupata haki. Unapoamua kumwamini Kristo, maana yake umeamua kugeuka na kuachana na mambo ya gizani. Unapoamua kumwamini Kristo maana yake lazima utapata haki kwa njia ya imani kupiti Kristo YESU.

Lakini hakuishia hapo …akasema na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Hapa unapokiri unakiri nini??

Tuelewane hapa; anaposema mtu hukiri hata kupata wokovu, lazima ujue unakiri nin?? Tunaokolewa kwa njia ya imani kupitia Yesu Kristo... ukiamini kwamba Yesu alikufa na akafufuka kutoka kwa wafu uwe na uhakika utahesabiwa haki mbele za Mungu.

Lakini sasa mbona akasema tena kukiri hata kupata wokovu. Kiukweli kuamini tu kazi ya msalaba inatosha kabisa kuhesabiwa haki lakini tunatakiwa kukiri, lazima ukubali kuwa ulikuwa mdhambi lazima umwambie Mungu kuwa ulikuwa mtenda dhambi, kubali kwanza ndo kitu Mungu anachotaka.

Lakin unakiri vipii? ...hebu tuangalie hapa; Yeremia 8:6; *"Nalisikiliza nikasikia, lakini walisema yasiyo sawa; hapana mtu aliyetubia maovu yake, akisema, Nimefanya nini? Kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe, kama farasi aendavyo kasi vitani."*

Haya maneno Mungu alikuwa anasema na Jeremiah na mistari miwili ya juu ndo utaelewa kwanin Mungu alisema maneno haya... Mungu anasema naliskiliza nikaskia mbona hasema naliskiliza nikaskiliza ila anasema nalisikiliza nikaskia.

Kumbe kuna tofauti kati ya kuskiliza na kuskia...

Tofauti yake ni ipi? mtumishi napenda kujua zaidi hapa.

Jambo lolote ambalo umeskiliza likaleta impact ndani yako maana umeskia.

Kusikia ni ndani na kuskiliza ni nje; unaweza ukaskiliza lakini usisikie …maana yake ni hii kwa mfano umepita sehemu ukaskia mziki unapigwa. Ukiona wewe unaanza kuuimba moyoni maana yake umeskia ila kama ulisikiliza halafu hauumbi moyoni maana yake uliskiliza hukusikia.

Jambo lolote ambalo umesikiliza na halijaleta impact ndani yako maana umesikiliza. Kwa lugha nyingine kuskia maana yake kutii angalia andiko hili hapa...

Kumbukumbu la Torati 28:1; *"Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;"*

Ukisoma maandiko yanayofuata baada ya andiko hili ndo utaelewa maana ya kuskia. Hapo unaweza kutoa neno kuskia na kuweka kutii.

Mungu anaendelea kusema …lakini walisema yasio sawa. Hapana mtu anaetubia maovu yake. Anasema hakuna mtu anaesema kafanya nini kakosea nini kila mtu anajikanyaga tu wanakiri vitu visivyoeleweka mbele za Mungu.

Munga akawa hawaelewi halafu akasema kila mtu hurudia mwendo wake mwenyewe yaani kwa maana nyingine ni kwamba wanakiri makosa yao lakini wanayarudia tena na tena, hakuna ambae alikiri na akaamua kuacha na ndo maana akasema kila mtu hurudia mwenendo wake mwenyewe kama farasi aendavyo kasi vitani.

Yaani, jamaa wanaungama then wanarudia tena na tena na tena. Unaona Mungu anamwambia Yeremia, hawa watu siwaelewi ni toba gani wanafanya ambayo hawabadiliki?

Kwahiyo unapofanya toba kwanza, umeamua kwa kumaanisha, pili tamka makosa yako mbele za Mungu bila kuficha siyo kwamba Mungu hajui ulichofanya ila anataka ukiri wewe mwenyewe kwa kumaanisha siyo unaruka ruka tu hakuelewi.

Unapotubu amua kuwa mkweli mbele za Mungu. Na ukiwa unatubu kama humaanishi Mungu anajua maana yeye anajua mioyo yetu.

Wakorintho 7:10; *"Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti."*

Biblia inasema huzuni ya Mungu huleta toba iletayo wokovu; kivipi? chukua mfano wa Petro na Yuda.

Petro alimkana Yesu. Yuda alimsaliti Yesu. Wote hawa walikosea huo ndo ukweli. Na kila mmoja baada ya tukio lake alijua kua amekosea. Petro akaomba msamaha sana. Yuda akaumia sana na akaamua kurudisha zile pesa na baada ya hapo akaenda kujinyonga, lakini Petro je alijinyonga? la hasha…

Hii ndo maana ya huzuni itokanayo na Mungu na huzuni itokanayo na shetani. Huzuni ya Mungu itakupeleka kwenye toba ya kweli. Lakini ya shetani itakupeleka mautini.

Toba ni kwa ajili ya ondoleo la dhambi baada ya kugeuka na kuacha njia mbaya. Siku uliamua kuamini kazi ya msalaba ndo ilikuwa toba yako.

Kwa leo naishia hapa wapendwa naomba kama kuna mtu ana swali linalohusiana na mafundisho ya leo nimetoa nafasi ya maswali mpendwa ndani yangu naskia kutoa nafasi hiyo.

Je Kuna ukomo wa mtu kuomba Toba?  Especially aliyemjua Mungu lakini hasimami vizuri na Mungu na mtu huyu anaweza kusaidiwaje na je Kuna madhara yoyote anayoweza kuyapat?

Hutakiwi kufanya dhambi, neno linasema ivi aliezaliwa na Mungu hatendi dhambi bali anajilinda na hila za mwovu kujilinda sio kazi ya Mungu ni kazi yetu. Tunafananisha sana toba na rehema

Lakini Petro anasema hivi... 2 Petro 2:20-22; *"Kwa maana wale waliokwisha kuyakimbia machafu ya dunia kwa kumjua Bwana na Mwokozi Yesu Kristo, kama wakinaswa tena na kushindwa, hali yao ya mwisho imekuwa mbaya kuliko ile ya kwanza. Maana ingekuwa heri kwao kama wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu waliyopewa. Lakini imetukia kwao sawasawa na ile mithali ya kweli, Mbwa ameyarudia matapiko yake mwenyewe, na nguruwe aliyeoshwa amerudi kugaa-gaa matopeni."*

Kwahiyo toba ni mara moja tu ila rehema haina idadi. Tusifanye makosa ya maksudi kwa kigezo cha kuomba rehema kila siku. Kuna watu wanaishi maisha ya kutubu kila siku. Wakati mwingine mtu anaomba msamaha kwa makosa ambayo alishasamehewa tayari.

Unajua kwamba Yesu alishasamehe hata dhambi za kesho? Anyways, kama hujaelewa hii sentensi ni kwamba wakati Yesu anakufa na kufufuka kwa ajili ya dhambi zetu nani alikuwepo kati yetu?

Neno linasema alifanyika dhambi ili sisi tuweje?...

Ukiamini tu unahesabiwa haki hapohapo, hakuna habari za kesho wala badae. Hata kama ndo umetoka kuua then ukaamini kazi ya msalaba hapo hapo unahesabiwa haki. Na hii ndiyo toba sasa, maana ni kukubali na kuamua kuhama ufalme.

 

Tuandikie 'Maoni Yako' Hapa
Share :
Facebook Twitter

 

ads

Back To Top